Hii kwa ajili ya ndugu zangu wote wanao tafuta kazi kwa mda mrefu sasa !
Naanza kwa kutoa pole kwa Changamoto iliyopo kubwa ya Ajira Duniani na si Tanzania tu, Tumesoma na kuhitimu masomo yetu tukiwa tukijua baada ya shule ni kazi.
Kwenye soko la Ajira la Nchi yetu Tanzania bado lina nafasi nyingi sana za kazi watu wengi wanaweza kushaangaa kwa nini nasema hili.
Changamoto yetu sisi Candidates tunaendelea kutumia njia zile zile za mwaka 1990 kutafuta kazi.......Njia ya kutuma CV na kusubiri kuitwa kwenye INTERVIEW inaweza ikawa bado inafanya kazi lakini bado tunahitaji njia mpya kwani mambo kwa sasa yamebadilika sana !
Kwa yeyote anaesoma post hii na anatafuta kazi, cha kwanza kabsa akubali kuiweka CV yake nyuma bali yeye awe Mbele ya CV yake......Maana yake ni kwamba usiwaze napataje kazi ile waza nahitaji kuwa nani ili napite ile kazi. You Need to Become First !
Sasa ivi wafanyakazi maofisini wanapunguzwa kila siku lakini kuna watu maofisini kwa namna yeyote hawawezi kupunguzwa labda kampuni ifungwe waza kwa nini wengine wanapunguzwa na wewe unaomba kazi usije ukaipata na wewe ukakatuna fimbo ya kupunguzwa baada ya mwezi !
Ushauri wangu kwa yeyote huko nje ni kwamba sasa hivi badilisha approach, kaa chini fikiria kwa kina unatamani siku moja ufanye kazi @mwananchi_official Ebu waza kwenye sekta ambayo unataka kuomba hawa watu wana changamoto gani kwa sasa then waza na uje na jibu kama ni masoko ebu andaa majawabu yao ya Masoko then omba appointment ya kumwona Marketing Director/Mtu yeyote anaehusika mwambie nina Majawabu kwa nini unapata taabu kwenye Soko hapa lazima akupe sikio na unafanya presentation yako baada ya kuwapa majibu watakuomba CV yako baada ya hapo unaitwa kwenda kutatua TATIZO lao ofisini hautapunguzwa kazini !
Hii Courage inaambatana na kujiamini, kuwa na taarifa za kutosha, kuwa mbele kila siku, kuwa na mawazo chanya, kuwa mnyenyekevu, kuwa mbishi mwenye tija/aggressive with purpose, kuwa mwenye maarifa sahihi na haya yote yanapatikana kwa kujifunza mwenyewe wakati ukiwaza natakiwa kuwa nani ili niipate kazi fulani na si niandikaje CV yangu !
#MrBrand
#Read2Lead
#Imeandikwa Na Charles Nduku
#Imesambazwa Na kinguswaz.blogspot.com
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA