Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli leo tarehe 27 Oktoba, 2017 saa 8:00 mchana atawaapisha Makatibu
Wakuu wapya, Naibu Makatibu Wakuu
wapya na Wakuu wa Mikoa wapya baada ya jana tarehe 26 Oktoba, 2017 kufanya
mabadiliko katika safu ya uongozi wa
nyadhifa hizo.
Kufuatia mabadiliko hayo safu ya
Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu
Wakuu itakuwa kama ifuatavyo;
Ofisi ya Rais Ikulu.Katibu Mkuu – Bw.
Alphayo KidataOfisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora.
Katibu Mkuu ( Utumishi ) – Dkt.
Laurian NdumbaroNaibu Katibu Mkuu – Dorothy Mwaluko (ATAAPISHWA)Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI ).
Katibu Mkuu –
Mhandisi Mussa IyombeNaibu Katibu Mkuu( Afya ) – Dkt. Zainabu ChaulaNaibu Katibu Mkuu( Elimu ) – Bw. Tixon
Nzunda Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.Katibu Mkuu – Mhandisi Joseph Kizito Malongo (ATAAPISHWA)Naibu Katibu Mkuu – Bi.
Butamo Kasuka Phillipo (ATAAPISHWA)Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu.Katibu Mkuu( Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu ) – Bw. Erick
ShitindiKatibu Mkuu( Bunge na Waziri Mkuu ) – Maimuna TarishiKatibu Mkuu(Sera na Uratibu ) – Prof. Faustine
KamuzoraWizara ya Kilimo.Katibu Mkuu – Mhandisi Methew MtigumweNaibu Katibu Mkuu – Dkt. Thomas Didimu
Kashililah (ATAAPISHWA)Wizara ya
Mifugo na Uvuvi.Katibu Mkuu ( Mifugo) –
Dkt. Maria MashingoKatibu Mkuu (Uvuvi ) – Dkt. Yohana BudebaWizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano.Katibu Mkuu (Ujenzi ) – Mhandisi Joseph
NyamuhangaKatibu Mkuu (Uchukuzi ) –
Dkt. Leonard ChamrihoKatibu Mkuu (Mawasiliano) – Dkt. Maria
SassaboNaibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Mhandisi Anjelina
MadeteWizara ya Fedha na
Mipango.Katibu Mkuu – Doto James
MgoshaNaibu Katibu Mkuu ( Utawala ) –
Bi. Susana Mkapa (ATAAPISHWA)Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) – Bi. Amina
ShaabanNaibu Katibu Mkuu (Sera ) –
Dkt. Khatibu KazunguWizara ya Nishati.Katibu Mkuu – Dkt. Hamis MwinyimvuaWizara ya Madini.Katibu Mkuu – Prof. Simon S. Msanjila (ATAAPISHWA)Wizara ya Katiba na Sheria.Katibu Mkuu – Prof. Sifuni MchomeNaibu Katibu Mkuu – Amon MpanjuWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.Katibu Mkuu – Prof. Adolf F. MkendaNaibu Katibu Mkuu – Balozi Ramadhani Muombwa MwinyiWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.Katibu Mkuu
– Dkt. Florence TurukaNaibu Katibu Mkuu – Bi. Immaculate Peter NgwaleWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Katibu Mkuu – Meja Jen. Projest RwegasiraNaibu Katibu Mkuu – Balozi Hassan Simba YahayaWizara ya Maliasili na Utalii.Katibu Mkuu – Meja Jen. Gaudence MilanziNaibu Katibu Mkuu – Dkt. Aloyce K. NzukiWizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya MakaziKatibu Mkuu – Dorothy Mwanyika (ATAAPISHWA)Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Moses M. KusilukaWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.Katibu Mkuu – Prof. Elisante Ole GabrielNaibu Katibu Mkuu (Viwanda ) – Ludovick J. Nduhiye (ATAAPISHWA)Naibu Katibu Mkuu ( Biashara na Uwekezaji ) – Prof. Joseph Buchwaishaija (ATAAPISHWA)Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.Katibu Mkuu – Dkt. Leonard AkwilapoNaibu Katibu Mkuu – Prof. James Epiphan MdoeNaibu Katibu Mkuu – Dkt. Ave-Maria SemakafuWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Katibu Mkuu ( Afya) – Dkt. Mpoki UlisubisyaKatibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ) – Bi. Sihaba Nkinga.Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katibu Mkuu – Bi. Suzan Paul Mlawi (ATAAPISHWA)Naibu Katibu Mkuu – Nicholaus B. William (ATAAPISHWA)Wizara ya Maji na Umwagiliaji.Katibu Mkuu – Prof. Kitila MkumboNaibu Katibu Mkuu – Mhandisi Emmanuel Kalobelo
Mhe. Rais Magufuli atawaapisha Wakuu wa Mkoa 6 aliwateua jana kama ifuatavyo;
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mnyeti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Joel Bendera ambaye amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Wangabo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na anachukua nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Bw. Adam Kigoma Malima anachukua nafasi ya Dkt. Charles Mlingwa.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bi. Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini na anachukua nafasi ya Bw. Jordan Rugimbana.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Bw. Byakanwa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na anachukua nafasi ya Bi. Halima Dendego.
Tukio la kuapishwa kwa viongozi hawa litarushwa moja kwa moja (Live) kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam kupitia vyombo vya habari vya Redio na Televisheni pamoja na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA