ALICHO KIANDIKA HAMIS KIGWANGALA ULINZI ZAIDI


Juzi tulifanikiwa kumkamata Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. Amekutwa na risasi 356, magazines 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha! ‬ Tutaendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili. 

Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini. Tunajua mnyororo wa ujangili unapoanzia (kwa maskini kama hawa akina Masalu) na kuishia kwa vinara wenye fedha nyingi, mamlaka na majina makubwa kwenye biashara na siasa, ndani na nje ya serikali, na kuishia kwa wafanyabiashara wa kimataifa, na ninawahakikishia tutawafikia na cha moto watakiona! Hatutoangalia sura wala jina, wala cheo wala itikadi yake kisiasa. Tutasimamia sheria tu. #HK #MzeeWaField #SiasaNiVitendo 

Comments