Beyonce amethibitisha kushiriki (kuingiza sauti) katika ujio mpya wa filamu maarufu ya mwaka 1994 "The Lion King" iliyochezwa kwa muundo wa Uhuishaji (Animation), huku Queen Bey akitajwa kucheza uhusika wa Nala.
Kampuni inayohusika kuandaa filamu hiyo 'Disney', leo imeachia list ya Waigizaji wote wa filamu hiyo iliyowahi kujizolea umaarufu mkubwa duniani, huku ushiriki wa #Beyonce ukipokelewa kwa furaha zaidi na wapenzi wa filamu.
Washiriki wengine ni Donald Glover atacheza uhusika wa Simba, na James Earl Jones akimvaa Mufasa, na Alfre Woodard akicheza kama Sarabi.
Mchekeshaji Billy Eichner na Seth Rogen watacheza kama Timon and Pumbaa respectively, huku John Oliver akimvaa Zazu.
Filamu hiyo imepangwa kuachiwa Julai 19, 2019 na itaongozwa na Muongozaji Jon Favreau.
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA