Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kusema kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Katika uamuzi wake, Hakimu Simba amesema amepitia hoja zote za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu hoja za kupokelewa ama kutopokelewa kielelezo hicho, ambapo ameona akipokee.
“Mahakama inatupilia mbali pingamizi la utetezi la kutaka kielelezo kisipokelewe, hivyo nimekubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kielelezo kinapokelewa,”
Hakimu Simba amesema sababu za kupokea kielelezo hicho ni kwamba Wema hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake bali ni nyumba yake, hivyo haina tatizo kama ilipekuliwa na askari wakiume.
” Kama upekuzi ungeusu maungo ya mwili wake basi kungekuwa na tatizo, lakini umefanyika nyumbani kwake,”.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi November 16/2017.
Mbali ya Wema katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA