Msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shabani ‘Keisha’ amefunguka kuwa, anatarajia kurudi kwa kishindo kwenye gemu ila ujio wake hauna uhusiano na kusambaa kwa picha za ndoa ya msanii Dogo Janja ‘Janjaro’ na Irene Uwoya.
Akipiga stori na Full Shangwe Keisha alisema, anatarajia kurudi kwa kishindo hivi punde kwenye gemu lakini kazi yake haina uhusiano wowote na kusambaa kwa picha za harusi ya Dogo Janja na Uwoya bali watu wanamzushia tu. “Ni kweli narudi kwenye muziki lakini ujio wangu hauna uhusiano kwa namna yoyote ile na kusambaa kwa picha za harusi za Janjaro na Uwoya.
Mimi ni Muislamu safi, kamwe nisingeweza kukubali kuhusisha mambo matakatifu ya dini na vitu vya kidunia, watu waache kuzusha kuwa ni maandalizi ya video yangu mpya,”alisema
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA