Msichana mmoja katika mji wa Dera Ismail Khan nchini Pakistan ametembezwa uchi wa mnyama mbele ya mamia ya wanakijiji ili kufidia adhabu ya kaka yake aliyezini na msichana mdogo kiumri mwaka 2015.
Taarifa kutoka kwenye gazeti la Tribune la nchini humo zinaeleza kuwa kaka wa msichana huyo aliyetembezwa akiwa uchi, alifanya mapenzi na binti wa familia nyingine hivyo baraza la kijiji liliamuru kaka huyo alipe kiasi cha rupia 150,000 za Pakistan sawa na Tsh milioni 2.2 mwaka jana ili kuyamaliza matatizo hayo kifamilia.
Hata hivyo familia ya Mwanaume huyo mzinifu aliyetambulika kwa jina la Sajjad ilishindwa kutoa fedha hizo ndipo baraza hilo la kijiji lijulikanalo kama (Panchayati) lilipotoa hukumu hiyo ya kumtembeza dada wa Sajjad uchi wa mnyama mbele ya wanakijiji ili liwe funzo kwa familia nyingine.
Tayari polisi nchini Pakistan wametangaza kuwakamata watu saba kufuatia tukio hilo la udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia, wengi wa waliokamatwa ni viongozi wa baraza la kijiji waliotoa hukumu hiyo.
Matukio kama hayo sio mageni nchini Pakistan hii kutokana na msimamo na maamuzi makali ya mabaraza ya vijiji nchini humo kuwakandamiza wanawake.
Mwaka 2002 kulitokea hukumu ya ajabu kama hiyo ambapo mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Mukhtar Mai aliamriwa kubakwa na kundi la vijana ingawaje alienda kutoa taarifa mapema Polisi.
Mabaraza ya vijiji nchini humo yamekuwa yakitumika kusuluhisha kesi mbalimbali kwenye jamii huku yakilaumu kuwa mahakama nchini humo ni dhaifu katika utendaji ingawaje serikali nchini pakistani haitambui uwepo wa mabaraza hayo.
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA