KAMA kuna watu wanambeza Laudit Mavugo, basi imekula kwao, kwani straika huyo Mrundi kwa tizi alilokuwa akilipiga kwenye mazoezini ya timu hiyo kujiandaa na mchezo wao wa Jumapili, linaonyesha wazi amerudi kwenye fomu.
Simba inaifuata Mbeya City leo Ijumaa kwa ndege, ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza pointi mbili muhimu mbele ya watani zao Yanga Jumamosi iliyopita, lakini jinsi Mavugo alivyojinoa ni kama ametuma salamu Mbeya.
Simba ilikuwa ikifanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini chini ya makocha Joseph Omog na msaidizi wake Masudi Djuma.
Tangu Jumatatu wiki hii Simba ilipoanza tizi kujiandaa na pambano lao la Mbeya City, mwandishi aliweka kambi na kushuhudia vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakipiga mazoezi ya kufa mtu.
Hata hivyo katika mazoezi hayo imethibitika kuwa, straika Laudit Mavugo anarudi baada ya kuyumba tangu atue Msimbazi akitokea Vital’ O ya Burundi.
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA