RICH MAVOKO - HAKUNA MSANII WA 'WCB' ALIYEPEWA GARI NA WCB .

Rich Mavoko afichua siri ya wasanii wa label ya 'Wasafi Classic Baby' kuzawadiwa Magari kwenye Birthday zao

Baada ya kusubiliwa kwa hamu ni lini na yeye atakabidhiwa Gari kwenye Birthday yake kama ilivyofanyika kwa Harmonize (Mark X) na Rayvanny (Rav 4), Rich Mavoko amefunguka na kusema kuwa hakuna msanii aliyepewa Gari na WCB .
.
. "Lifestyle yangu ipo tofauti nina gari lakini gari sio kitu ambacho napenda sana mimi napenda sana majumba majumba kwahiyo watu kupewa gari ni kwamba hupewi, utapewa viongozi watajua wanakatana nae vipi kwahiyo mimi sikuwahi kusema eti nimepewa gari na wcb ila nimeshapewa gari na wcb ila sikuwahi kutangaza wala sikuwahi kuposti na sina mpango huo" amesema @Richmavoko .
.
.

Harmonize na Rayvanny ndio wasanii pekee wa WCB waliopewa magari hadharani na uongozi wa label hiyo

Comments