Sethi, Rugemarila waendelea kusota rumande

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana ijumaa Novemba 24 2017, imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara, James Rugemarila hadi Desemba 8, 2017, kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Upande wa mashtaka umemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa wanaomba upelelezi ukamilike kwa haraka kwasababu hali ya mshtakiwa mmoja si nzuri.

Harbinder Singh Sethi pamoja na Mfanyabiashara James Rugemarila, kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya zaidi ya Bilioni 3.

Comments