JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI?
Neno la Msingi:
Zaburi 101:3
Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.
Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya "AIBU" wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni. Wanaume wamejikuta wakipiga punyeto (Mastubation) na Wanawake wakijisaga ( wanatumia mikono yao na viungo vyao vingine kama njia ya kujikidhi hali zao za tamaa mbaya waliloziamsha wao wenyewe).
Haipaswi kamwe kuwa hivyo. Biblia inasema tusiyachochee wala kuyaamsha "mapenzi" mpaka yatakavyoona yenyewe (Wimbo ulio bora 2:7, 3:5). Naomba tufuatane pamoja kwenye somo hili muhimu sana ambalo litakuweka huru mbali na "utumwa wa fikra za kingono"
MAANA YA PICHA ZA NGONO
Neno PICHA ni kivuli cha mtu, watu, kitu n.k. PICHA si kitu halisi bali ni kivuli chake.
Unaweza ukapewa PICHA ya mtu lakini usifahamu urefu wake au ni mfupi kiasi gani lakini sura yake ukawa umeiweka katika kumbukumbu yako. NGONO ni kitendo cha mtu, watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama.
Kuangalia picha za ngono ni kitendo cha kuangalia watu wakifanya Matendo ya kujamiana iwe kwa njia ya asili, kinyume na maumbile au kufanya na wanayama.
Kitendo hicho huleta kuchochea tamaa ya miili kiasi ambacho watu wengine hufanya mambo ya "AIBU" katika nyumba zao (Warumi 1:24-28).
PICHA za NGONO zimeenea kila mahali kwa sasa, kwenye simu yako unaweza ukakutana na "uchafu" wa namna hiyo.
Wahindi wao picha za ngono huziita "kachumbali" na unaweza ukamkuta Mhindi amekaa na familia yake anaangalia "kachumbali" wanadai inanogesha utamu wanapofika kitandani.
Huko ni kujidanganya Mungu hakumletea Adamu PICHA ya NGONO bali alimletea mke ambaye watashirikiana naye kwenye Tendo Takatifu (Mwanzo 2:18, 21-25).
Wakati mmoja Mfalme Daudi wakati watu wake wa vita wamekwenda vitani yeye akawa yuko ghorofani anaangalia "PICHA LIVE" ya NGONO mwanamke alikuwa akioga matokeo yake yakawa ni kufanya kitendo chenyewe na kuamua kumuua mume wa Bathsheba (2Samweli 11:2-27.
Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.
Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?………..
Kile kitendo cha Daudi "kuona" lilikuwa kosa kubwa la kiufundi katika akili yake likamchanganya.
Ndivyo ilivyo kwa PICHA ZA NGONO lazima ukiangalia upate "UKICHAA" wa muda ukajikuta umeng'ang'ania sabuni au ndizi ukiwa unapiga punyeto.
Ni aibu sana sana mtu mwenye heshima zako kama wewe labda wewe ni meneja, mkurugenzi, mtu mwenye Elimu yako ya maana unakutwa unaangaika sabuni, godoro au toy la jinsia ya kiume.
JE ! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI ?
Kuangalia picha za ngono "NI DHAMBI" kwa herufi kubwa.
Katika Sheria ya Musa ilikuwa mtu anahesabika kuwa ametenda dhambi pale ambapo atakutwa akifanya kitendo hicho au kukiwa na mashahidi wawili au watatu atatakiwa kuhukumiwa sawasawa na Sheria husika.
Kwenye dhambi ya uzinzi mtu alitakiwa apigwe mawe hadi afe sivyo kwa Sheria ya Kristo yenyewe inazungumzia juu ya kitendo cha "kutamani" tu unahesabika kuwa umefanyika DHAMBI (Mathayo 6:27-29, Waebrania 10:28).
Tamaa mbaya ni dhambi kama dhambi nyinginezo. Kwa kawaida tamaa huja na ile tamaa huchukua mimba na baadaye huzaa dhambi (Yakobo 1:13-16).
Kitendo cha kuangalia picha za ngono hupofusha "FIKRA" nzuri za mtu alizonazo.
Mawazo machafu uanza kutawala katika ubongo wako hadi "USHUSHE" huo mzigo ulioko kwenye viungo vyako vya uzazi. Ahaaa ni hatari aiseeee.
Wewe unayengalia picha za ngono Kama ndiyo starehe yako unaiharibi nafsi yako "unakuwa zezeta wa akili" Biblia inasema "taa ya Mwili jicho na jicho lako likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru.
Lakini jicho lako likiwa bovu mwili wako wote utakuwa na giza.."(Mathayo 6:22-23).
Kwa wale wanandoa ni "MWIKO" kutumia picha za ngono ili kunogesha kufanya Tendo la Ndoa. Wewe mume unaye hapo "chombo" unakiona "live" na kimethibitishwa na Mungu mwenyewe sasa hiyo mipicha ya nini? Kila kiungo Mungu alikiweka kwa ajili ya kusudi maalum kama ni mdomo kwa ajili ya kuongea na kupitisha chakula na si kunyonya sehemu za Siri za mwenzi wako.
Mungu ameweka sehemu ya "haja kubwa" kwa ajili ya kutolea uchafu uliotengenezwa na tumbo na si kiungo kingine kiende kukoroga "zege" hilo huo ni uchafu(Ufunuo 22:10-15).
Warumi 1:26:27
Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
PICHA ZA NGONO zinavutia sana kuziangalia ila zina maangamizo makubwa sana katika maisha yako.
Lazima ufikie mahali kukata shauri ndani ya Moyo wako kuambatana na Mungu. Kusudi kubwa la shetani kuachilia mambo yake ya NGONO kwenye mitandao ili apate wafuasi wengi zaidi.
Hakuna kitu unachoweza kukifanya katika simu za Android wengine wasikitambue.
Kila unalolipitia na kuliangalia kwa Siri siku ya siku litaletwa hukumuni na Mungu mwenyewe (Warumi 2:16, Mhubiri 12:14)
USHAURI WAKIVITENDO:
I) Yatie Nuru macho yako - Zaburi 13:3, 19:8 - Yaruhusu macho yako yaingiziwe nuru na Yesu.
Chukua muda wa kutosha kuingiza PICHA zinazomhusu Mungu zaidi. Angalia wahubiri mbalimbali.
II) Tazama mambo ya Adili(mema) - Zaburi 17:2-3 - Kuna nguvu kubwa sana tunapokuwa tunaangalia mambo mema.
Vipindi vizuri vya neno la Mungu.
PICHA zinazojenga siyo zinazoharibu fikra zetu.
III) Kumuomba Mungu afumbue macho yako - Zaburi 119:18, 146:8- Maombi ni muhimu ili kufanya macho yako kuona kusudi la Mungu na Kutambua uwepo wa shetani katika PICHA ZA NGONO.
IV) Weka maneno ya Mungu Mbele za macho yako - Mithali 4:20-21
Wakati wote soma neno la Mungu kupitia kifaa chochote cha ki-electronic ili uweze kumjua Mungu zaidi.
V) Macho yako yatazame Mbele - Mithali 4:25-27
Kutazama Mbele maana yake uwe na maono.
Maono ni PICHA au TASWIRA ya Mbele ya maisha yako.
Yeremia aliulizwa unaona nini naye akasema "anaona ufito wa mlozi" anaona kitu kizuri (Yeremia 1:11-12).
VI) Pendezwa na njia za Mungu - Mithali 23:26
Kuanzia sasa anza kupendezwa na njia za Mungu katika maisha yako.
Acha kuzifuata njia zako katika kuufurahisha mwili wako wa PICHA zisizofaa.
VII) Tafuta watumishi wa Mungu ili wakufundishe - Isaya 48:17, 30:20-21
Kuna mambo ambayo yanatupa shida katika maisha yetu ni vizuri kuwaona waalimu ili watusaidie jinsi ya kutoka katika mtego huo.
VIII) Omba rehema na neema ya Yesu - Waebrania 4:16
Tunahitaji neema ya Mungu ili kushinda Hali hiyo ya kupenda KUANGALIA PICHA ZA NGONO na pia kufunguliwa kutoka katika vifungo hivyo vya pepo wa tamaa na mahaba.
Mungu atakubariki ukipeleka ujumbe huu kwa wengine
NA MUNGU AKUBARIKI SANA
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA