1st: Greetings/Salamu: Pata wasaa wa kusalimia watu kwa njia ya text, simu, barua pepe na kama unaweza watembelee kabsa to be precise. Kila mwanzo wa wiki unaweza ukawa umetengeneza text yako inasema "Nakutakia week ya mafanikio Mr @mcndimbo_weddings "hii inakutuma ujumbe kuwa upo na upo pamoja na mtu husika. Kuna watu tuna namba zao hata akipiga jina linatokea lakini humukumbuki kabsa. Jenga utamaduni wa kuwajulia hali your potential network.
2nd: Wishes/Kuwatakia kheri. Unalifanya kwenye Vipindi mbalimbali kama birthday, anniversary, uteuzi, wedding, na nk. Hii inapeleka ujumbe wa kimya kimya kuwa unapenda Maendeleo ya wengine kwa kufurahia nao.
3rd: Sympathy/Pole: Kila mwanadamu anapitia magumu kwenye namna tofauti inawezekana ikawa kwenye level ya taasisi au mtu binafsi, katika Vipindi kama hivi do not miss a point ya kusema pole, inawezekana ikawa Msiba, Kutenguliwa, magonjwa, any loss. Hapa utakuwa unajichukulia point tatu za mezani kabsa.
4th: Appreciations/Recognition/Kumshukuru na kutambua. Appreciation is the human need, kila mwanadamu anahitaji kushukuriwa kwa namna gani anaongeza thamani kwenye maisha ya wengine. Pata wakati wa kumtumia ujumbe, mpigie simu, au unaweza kumwambia MTU mwingine wa karbu kwa namna gani anagusa maisha yako, au kwa namna gani unajifunza kwake. Hii inaongeza nguvu sana upande wa mahusiano. Kama una nafasi unaweza kupeleka kitu kama zawadi. Mahusiano ni uwekezaji.
5th: Jitahidi mwanzoni wa mahusiano usijenge picha mbaya kwani kuna watu simu zao zikipigwa tunaweza kutabiri wanataka kusema nini. Hakikisha watu wasikutabiri huwa unapiga simu Mara zote kulalamika au kuomba kitu. Siku zingine unapiga simu kutoa fursa kwao. Na hii itakusaidia kukuza urafiki.
Mahusiano ni gharama kwahiyo mahusiano ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine kwani atlast watu wanapenda kufanya biashara na watu wanaowajua na kuwaamini sasa ni ngumu kukujua kama huwezi kuwekeza kwenye hisia za wengine. #MrBrandGroup
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA