Hivi vitu visikupe shida katika kufuata ndoto zako:

1st: Internet should not rush you. Mtandaoni Mara nyingi watu tunapost mafanikio tu ila hatupost failures unaweza ukaangalia mtandaoni na ukapata presha kubwa, Ukaona kama wewe ndiyo vitu vyako haviendi. Hold on and trust the process. 2nd: Marafiki: Kuchelewa kufikia hatua ambayo rafiki ama mtu wa karbu amepata si tatizo kila mmoja ana Baraka zake na njia zake za pekee. Usijilinganishe kwa kusema why not me ila jilinganishe kwa kujichallenge na kusema acha na Mimi niongeze nguvu kumbe inawezekana. 3rd: Time: Huwezi kupanda mbegu na siku hiyohiyo ukavuna, kwenye maisha kuna majirani na nyakati sahihi. Kila kipindi ni cha dhahabu Sana. Kibinadamu Ni ngumu kuelewa lakini Mungu analo kusudi la wewe kusubiria ama kuchelewa na mwisho wetu lazima uwe na matokeo chanya. Tujifunze kuaamini katika majira na wakati sahihi wa Mungu ambao sisi tuendelee kuamini kwenye ibada ya UVUMILIVU. 4th: Umri: Mimi nafikiri hakuna umri sahihi wa kufanikiwa ila jitihada zetu tu kwenye umri wowote tulio nao sasa tunaweza kubadilisha Dunia ama Matokeo. Umri si kipimo Cha mafanikio ila jitihada zetu ndyo kipimo sahihi. Wengine wanafikia umri fulani na kuamini kuwa hapa ndiyo mwisho si kweli. Age is Number and Efforts never lie. Imeandikwa Na Charles Nduku #MrBrand FOR ADVERTISES CALL US KAMA UNA NYIMBO BIASHARA YOYOTE ILE HALALI TANGAZA HAPA SASA

Comments