Lilikuwa swali la shabiki kwenda kwa Joh makini moja kwa moja kwenye #Planetbongo akitaka kujua kuhusu tetesi za muda mrefu kuwa wana bifu na rapa mwenzake kutoka mwanza Farid kubanda #FidQ.
Joh makini alijibu kwa kucheka huku akitania "...inaonekana nyie jamaa mkikaa maskani mnaunda mapichapicha sana eh?..." Alitania joh kwasababu swali moja kabla ya hapo liliulizwa na shabiki mwingine kuhusu uwepo wa bifu kati ya kundi analotoka joh makini #RiverCampSoldiers na #Nako2Nako ambapo alikanuaha kuwahi kuwepo kwa bifu.
Sasa kuhusu fid Q,Joh makini amesema hakuna bifu yoyote kati yao ila ni maneno tu ya watu/mashabiki ambao uamua kutengeneza story za aina hiyo kuonyesha kuna bifu baina ya wasanii.
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA