Akizunguma leo Mbunge wa Kibamba John Mnyika amesema kwa kawaida mkutano wa uchaguzi hautakiwi kuitishwa kwa mtindo wa dharura.
By Josephat Charles
Akizunguma leo Mbunge wa Kibamba John Mnyika amesema kwa kawaida mkutano wa uchaguzi hautakiwi kuitishwa kwa mtindo wa dharura.
Dar es Salaam. Uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Ubungo umeshindwa kufanyika baada ya madiwani wa Chadema kususia uchaguzi huo na kudai kuwa hawakupewa taarifa mapema na badala yake walitaarifiwa juzi badala ya kipindi kisichopungua wiki moja.
Akizunguma leo Mbunge wa Kibamba John Mnyika amesema kwa kawaida mkutano wa uchaguzi hautakiwi kuitishwa kwa mtindo wa dharura.
Amesema Mkurugenzi wa Manispaa hiyo alitakiwa kuwajulisha madiwani hao mapema na siyo juzi kama alivyofanya. Amesema pia Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Akson amepelekwa kupiga kura Kinondoni wakati ni mkazi wa Kibamba.Amesema pia Diwani wa Kata ya Saranga wilaya ya Ubungo, Frolence Masunga amepelekwa kupiga kura Kinondoni.
"Tumekataa uchaguzi usifanyike ingawa tungeshinda.Tunataka Raid John Magufuli afahamu mizengwe wanayotaka kuifanya ili kushinda kiti cha Umeya Kinondoni".alisema Mnyika
Mkurugenzi wa Manispàa ya Ubungo John Kayombo amekataa kuzungumza na wanahabari kuhusu kuvunjika kwa mkutano huo.
"Mnataka niongee nini Mimi nimeshamaliza watafuteni maofisa uhusiano ndiyo wasemaji"alisema huku akiingia ndani ya gari na kuondoka.
Madiwani wa chadema wameondoka kuelekea Kinondoni na wale wa CCM wamekwenda majumbani. wameondoka kuelekea Kinondoni na wale wa CCM wametata
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA