Makamba: Mazingira yatawaadhibu watanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema ni dhambi kubwa kuharibu mazingira ambayo mwisho wa siku hayatakusamehe bali yatakuadhibu.

By Josephat charles

Makamba ameeleza hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Lubanda wilayani Ileje mkoa mpya wa Songwe.

Ileje.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema ni dhambi kubwa kuharibu mazingira ambayo mwisho wa siku hayatakusamehe bali yatakuadhib
Makamba ameeleza hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Lubanda wilayani Ileje mkoa mpya wa Songwe.

Amesema ukimkosea binadamu mwenzako unaweza kusamehewa lakini ukiyakosea mazingira hayatakusamehe bali utasababisha uharibifu mkubwa mazingira.
"Ukitenda kosa unamwomba Mungu akusamehe.Lakini ukiharibu mazingira, hakuna msamaha bali utadhalilika.

"Nimelazimika kusema haya baada ya kujionea njiani uharibifu wa mazingira uliofanywa na baadhi yenu," alisema Makamba.

Alisema Ileje na Lubanda imebarikiwa milima, vyanzo vya maji na milima lakini kwa staili ya kuharibu mazingira inayofanywa itawapa wakati vizazi vijavyo.
Alieleza kuwa endapo mazingira yatatunzwa kwa ufanisi vizazi vijavyo vitaishi maisha maisha bora kwa kuwa kutakuwa na msingi bora wa utunzaji mazingira.

Comments