DIAMOND PLATNUMZ ANATAKA KUWAACHA VEVO

Ni muda sasa tangu staa wa muziki nchini, @DiamondPlatnumz kuweka wazi kuwa haoni haja ya kufanya kazi na @VEVO, kampuni ambayo inahusika na kuweka video mtandaoni kwani chaneli yake ya YouTube pekee inatosha.

Mawazo ya Diamond kwa sasa ni wazi yanaonekana kubadilika kwani nyimbo yake mpya ya #MarryYou ambayo amemshirikisha @NeYo ameiweka mtandaoni akiwa na chaneli ya VEVO jambo ambalo baadhi ya wadau wa muziki walishindwa kuelewa mwanzoni sababu awali Diamond aliwahi kusema haoni haja ya kufanya nao kazi.

Jumapili ya Februari, 26, Diamond kupitia akaunti yake ya Instagram amefunguka jambo ambalo wengi hatulijui kuhusu yeye kufanya kazi na VEVO. “Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo… Nikawambia:

“uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo…na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo”…..hivyo nikawambia: “siku mimi nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida….

SABABU YA KUYASEMA HAYA:

Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa
Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani

kuwawako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…” kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili

Comments