UOGA
Uoga ni hali ya wasiwasi ambayo kila mwanadamu anayo kwenye maisha yake, lakini hali hii isiwe ya kiwango cha juu kiasi kwamba kila kitu unachotaka kukifanya au kufanyia unatanguliza UOGA kama silaha ya kukwepea.
Vijana wengi sana nikiwemo mimi hapo awali nilikuwa naogopa sana kujaribu na kufanya baadhi ya mambo nikihisi nitakosea, nitaonekana sijui, watu wengine watanionaje nisipo patia, lakini nimekuja kugundua kuwa UOGA ndiyo daraja pekee linalotenganisha MAFANIKIO ya kila moja wetu.
Ndoto zetu na mipango imegawanishwa ni kitu kinaitwa UOGA, labda kwa sababu wengi wetu tulilelewa hivo kila kitu mpaka wazazi au walezi wakuuruhusu, ukitaka hata kubadilisha nguo utotoni ilikuwa mpaka umwulize mlezi au mkubwa wako, hii imetujengea hali fulani kubwa ya kutokujiamini katika maamuzi na kuwa na our THINKING kama vijana.
Ombi langy kubwa leo hii popote ulipo sasa hivi sema mimi siogopi chochote nitafanya kile ambacho naona nakiweza unless sivunji sheria za nchi, nitaamua kile ambacho nataka kufanya, nitaenda popote na nitafanikiwa, ondoa sababu zote za kusema kwetu sisi maskini, mimi sijasoma, mimi siwezi, mimi kwetu hatujafanikiwa sema hapana songa mbele kimbiza malengo na ndoto bila kuangalia visingizio vya aina yeyote.
Ndoto, Malengo na Mafanikio yetu yapo mikononi mwetu pambana wewe ni mshindi acha kuwa muoga, uoga wako umasikini wako.
#Mrbrandtz
Wilfred Minzi Emmanuel Mabula Daud Sung'wa Jeremia Mahona Seth Raban Iddy Kirika By Charles Nduku
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA