FAHAMU AINA YA MARAFIKI MBALIMBALI AMBAO WAPO KATIKA MAKUNDI MATATU

Duniani hapa tunapoishi kuna makundi makuu matatu ya marafiki ambayo tunao leo au tutakuwa nao kesho:

Kundi namba moja, hawa wanaitwa "Confidant Friends" kundi hili ni marafiki wa kweli na wenye nia ya dhati ya kutaka kukuona wewe unapiga hatua moja mbele ya kimaendeleo na si vinginevyo, wanafurahi na wewe katika furaha, wanaumia na wewe katika maumivu, mnatembea wote katika milima yako......wako tayari kutoa vitu vyao kwa ajili yako......watakuja kukuona hospital kama unaumwa, wakuhumudia hata kama utakuwa gerezani......Hawa ni marafiki muhimu sana na wenye kubwa kwetu......ukiwa nao wawili au moja wewe umebarikiwa na hutarud nyuma.

Kundi la pili: Hawa wanaitwa "Constituent Friends" Hawa ni marafiki ambao wako na wewe kwa sababu unakitu ambacho na wao pia wanakitaka kutoka kwako.......wakimaliza kukipata au wakapata mtu mwingine mwenye kukifanya kitu hicho hicho kwenye ubora zaidi wako radhi kukuacha kwani wao hawako na wewe ila wako na kitu ulichonacho tu basi.
Unatakiwa kuwanao makini sana katika maisha.

Kundi la tatu: Hawa wanaitwa "Comrades" hawa ni aina ya marafiki ambao wao wanakuja kukupa support tu wakati ukiwa na changamoto, kama unaadui unapigana nae wao watakuja kukusaidia kumpga adui huyo baada ya mapigano kuisha wao huondoka, wakisikia una changamoto yeyote watakusaidia tu.

Changamoto kwetu lazima uwachambue marafiki ulionao leo kama ni Confidants, Constituents ama Comrades!!!

#mrbrandtz

Comments