NGUVU YA MAONO / POWER OF VISION

Maono/Vision maana yake nini...... ni picha ya akili/mental picture ya mwisho kabsa kwa kile unachokiwaza kukifikia maishani mwako.......mfano mzuri wa hili ni........

Kulikuwa na mafundi watatu walikuwa wanajenga.........kuna mtu moja akawauliza, akamuliza fundi namba moja, unajenga nini ndg yangu........fundi akajibu nina panga panga tu matofali......fundi wa pili akaulizwa unafanya nini.....akasema najenga tu UKUTA......fundi wa tatu akaulizwa, akasema mimi hapa najenga Cathedral/Kanisa kubwa la kusalia watu zaidi ya elfu moja........kati ya mafundi hawa mwenye Vision/maono ni yule fundi namba tatu aliyekuwa anajua na anapicha halisi na kile anachokifanya leo ambacho bado hakijafikia kuwa Kanisa.

Maono yanatusaidia katika maisha, ukijua wewe unataka siku moja umiliki Hospital ya kwako.......hata kama leo hauna hata jengo........Vision/Maono yatakufanya ukutane na watu wenye kukusaidia katika kuyatafasiri Maono yako.......Maono pia yanatusadia kuwa na FOCUS ya kile tunachokifanya........Maono pia yanatutia MoYO wa kusonga mbele hata kama kipindi cha sasa ni kigumu sana...........kwani Maono huwa yanapingana sana na uhalisia wa maisha yako ya sasa kwani unaweza leo ukawa unalala njaa wakati wewe unawaza siku moja uwe na kiwanda chako cha kusindika chakula........Maono yanatusaidia kupata watu sahihi katika maisha........Maono pia yanatupa Comfort/kututia moyo kwani yanakuambia hapa ulipo si pako wewe unapita tu kuelekea mahali kule penye haja ya moyo na akili zako............!!!!!!!

Ishi Maono yako leo wala usiyumbishwe na hali yako ya sasa hata kama huna kitu chochote endelea kufanya kitu kila siku chenye kujenga Maono yako........ukiwa unakata gogo kila shoka inashiriki katika kulidondosha gogo husika na si shoka ya mwisho ambayo watu wengi wanaamini wakati shoka ya kwanza nayo imechangia sana.

Songa mbele kwa kujiamini kabisa, jiamini na amini kile unachokifanya sasa.

#Mrbrandtz

Comments