CHID BENZ AKAMATWA TENA NA MADAWA YA KULEVYA

‪Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya‬
|
Watu saba akiwemo Chid Benz ambaye jina lake halisi ni Rashid Makwiro wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa wa kipolisi Ilala kufuatia msako uliofanyika ambapo wamekutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.

Hivi karibuni tu Chid Benz alikuwa ameanza kurejea katika kazi zake za kisanii ambapo alitoa wimbo wa Q Cheif akielezea mateso aliyopitia huku wengi wakiamini kuwa ameacha matumizi ya dawa hizo.

Aidha, amekuwa akishiriki matamasha mbalimbali ya muziki na afya yake ilianza kuonekana imeimarika, wengi wakifurahishwa na maendeleo hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 majira ya saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya. “Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema Hamduni.

Kamanda huyo alisema kwa baada ya kuwakamata vijana hao sasa wanajikita kusaka mtandao mzima unaohusika na biashara hiyo ili kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi yao

Comments