MWANAFUNZI ALIWA NA MAMBA AKIOGA MOROGORO

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwaya iliyopo Wilayani Ulanga mkoani Morogoro amefariki dunia baada ya kuvamiwa na mamba wakati akioga pamoja na wanafunzi wenzake mtoni.

Akizungumza na ITV Diwani wa kata ya Mwaya na diwani wa Kata ya Chirombolo wamesema matukio hayo yamekithiri zaidi katika kata hizo mbili hali inayopelekea wakazi wa kata hizo kushindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kuhofia kuvamiwa na mamba na kulazimisha wakazi wengi kulala mapema.

Kwa upande wao viongozi wa Wilaya ya Ulanga wakiwemo madiwani katika Halmashauri ya Ulanga, wanasema wameandaa mpango mkakati wa kuweza kudhibiti kero hiyo

Comments