Betty Mbereko na mwanaye, Farai Mbereko.
BETTY MBEREKO (40) mwanamke anayeishi Mwenezi huko Masvingo, Zimbabwe, ameolewa na mwanaye wa kumzaa aitwaye Farai Mbereko mwenye umri wa miaka 23.
Katika hali hiyo ambayo ilitokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Oktoba, mama huyo anategemea kupata mwanaye ambaye pia ni mjukuu wake. Mwanamke huyo amekuwa mjane kwa miaka 12 iliyopita ambapo amekuwa akiishi na mwanaye huyo.
Alithibitisha hivi karibuni kuwa ana ujauzito wa miezi sita na hivyo akaona afadhali “aolewe” na mwanaye kwani hakutaka kuolewa na mmoja wa wadogo wa marehemu mumewe, aliosema wanamtamani.
Betty aliishangaza mahakama ya kijijini kwake aliposema alianza kuzini na mwanaye miaka mitatu iliyopita. Alisema baada ya kutumia fedha nyingi kumsomesha Farai baada ya kifo cha mumewe, aliona ana haki ya kufaidi fedha ya mwanaye na si mwanamke mwingine.
“Tazama, nilihangaika kumsomesha mwanangu na hakuna aliyenisaidia. Sasa mwanangu anafanya kazi na watu wanasema nimefanya kosa. Acha nifaidi mazao ya jasho langu,” aliiambia mahakama hiyo.
Farai alisema yuko tayari kumwoa mama yake na atalipa mahari kwa babu na bibi zake, ambayo baba yake hakuimalizia.
“Nafahamu baba alikufa kabla ya kumalizia mahari; niko tayari kuilipa Ni yema kutangaza kinachotokea kwani watu lazima wafahamu kwamba ni mimi nilimpa ujauzito, bila hivyo watasema ni mzinifu,” alisema Farai.
Lakini kiongozi wa kijiji hicho, Nathan Muputirwa, anasema: “Hatuwezi kuruhusu hili litokee kijijini kwetu, kwani hii ni dalili mbaya. Hapo zamani watu hawa walistahili kuuawa lakini leo hii hatuwezi kwa sababu tunaogopa polisi.”
Aliwaonya wawili hao wavunje ndoa yao au waondoke kwenye kijiji hicho ambapo walichagua uamuzi wa pili, na tangu hapo wameondoka kijijini hapo.
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA