RC MALIMA ATAKA ZAO LA MUHOGO KUWA ZAO LA BIASHARA

Mkuu wa mkoa wa Mara Mheshimiwa Adam Malima ameahidi kufanyia kazi tafiti zaidi zao la muhogo ili kuinua kilimo hicho na kukifanya kuwa zao la biashara ili kukuza uchumi wa mkoa huo.

Malima ameyasema hayo leo ikiwa ni siku yake ya kwanza kuanza kazi ya kuutumikia mkoa wa Mara wakati akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wake kuhusiana na mkakati wa kukuza uchumi.

Malima alisema ikiwa wilaya ya Butiama ina rutuba nzuri na wananchi hulima kilimo cha muhogo na kupata mavuno ya kutosha ipo haja kurithisha wilaya mingine katika Mkoa huo ili kufanya zao hilo lilimwe kwa wingi kwa faida ya mkoa huo.

"Nimefurahi kuona Butiama wanalima zao hili na lina stawi vizuri hivyo kinachohitajika ni kufanya wilaya zingine kuiga mfano huo na kuanza kulima kilimo hiki cha muhogo", alisema Malima.

Aidha alisema ipo haja kwa viongozi kuanza kutoa elimu kwa wananchi ili kuelewa kuwa zao hilo si la chakula pekee bali ni la biadhara na linaweza kusaidia wananchi kujipatia kipato kwa wingi kupitia zao hilo.

"Naomba wananchi waelewe kuwa muhogo ni zao la biashara pia kama mkulima atalima magunia 100, basi magunia 90 yawe ya biashara 10 yawe ya chakula", alisema Malima.

Mheshimiwa Adam Kigoma Malima ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kushika nafasi ya Mheshimiwa Charles Mlingwa ambaye kwa Mujibu wa sheria amestaafu.

Comments