SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) YAOMBA RADHI KWA WATANZANIA WOTE




Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limewaomba radhi wateja wanaokosa huduma ya umeme.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Oktoba 28,2017 na ofisi ya uhusiano Tanesco makao makuu imesema sababu ni kuathirika kwa miundombinu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Tanesco imesema mvua imesababisha maeneo mengine kuwa vigumu kufikika kwa haraka.

“Mafundi wetu wanaendelea na jitihada usiku na mchana kuhakikisha huduma ya umeme inarejea katika maeneo yote nchini,” imesema taarifa hiyo.

Shirika hilo limesema litaendelea kutoa taarifa na limewaomba radhi wateja kwa usumbufu unaojitokeza.

Tanesco imetoa tahadhari kwa wananchi wasishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Wakati Tanesco likitoa taarifa hiyo, Jumatano Oktoba 25,2017 umeme ulikatika nchini nzima kutokana na hitilafu kwenye gridi ya Taifa.

Comments