RAYVANNY NA MZAZI MWENZIE FAHYVANNY NDIO BASI TENA

MZAZI MWENZIE FAHYVANNY
Baada ya kuweka picha yenye caption ya kuijiita single mother , mwanadada mrembo ambae pia ni video queen katika video mbalimbali lakini pia ambae alitokea katika video ya Rayvanny ya kwetu iliomfanya akatambulika zaidi.baada ya kutokea katika video hii wawili hao walijikuta wameingia katika mahusiano ya kimapenzi yaliyowapelekea mpaka kupata mtoto mmoja wa kiume.

Lakini wawili hao wameonekana wakisambaratika na kuachana kabisa baada ya kutupiana maneno katika kurasa zao za instagram.

Mwandada huyo baada ya kuweka picha hiyo , mzazi mwenzie Rayvanny aliamua kumjibu na kumwambia kuwa kwa sababu ajishajiita single mother anaomba abadilishe na jina lake la mwisho ambaol alikuwa akilitumia lililokuwa likimtuambulisha kuwa ni mpenzi wa Rayvanny.

Mwanadada huyo ambae alikuwa akijiita Fayvanny baada ya kuchukua jina la mwisho kutoka kwa Rayvanny ameombwa kubadilisha jina hilo na mzazi mwenzie huyo baada ya kusemekana kuwa wameachana.
Hata hivyo katika account ya instagram ya mwanadada huyo amebadilisha jina hilo na kujiita Fayma_96 na kufuta baadhi ya picha alizokuwa akipiga na mzazi mwenzie huyo, hata hivyo katiak ukurasa wa Rayvanny mwenyewe amefuta picha zote alizokuwa amepita na mzazi mwenzie ambae alikuwa akikaa nae katika nyumba moja kama mke na mume.

Fayhma na Rayvanny walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume anaejulikana kwa jina la Jaydan ambae umri wake hajafikisha hata mwaka mmoja tangu amezaliwa.

Mapenzi ya wasanii wengi yamekuwa yakiishia ukingoni na kuacha watoto wao wakilelewa katika mazingira mabovu.Kama wamegombana basi kama mashabiki wanawaomba waongee na kupatana ili kulea mtoto mabe bado ni mdogo mwenye huitaji wa malezi ya wazazi wote wawili.

Comments