WEMA SEPETU KUONDOKA CHADEMA, ARUDI CCM


Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ametangaza rasmi kujivua uanachama wa Chadema na kurudi kwenye chama chake cha zamani cha CCM.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema Sepetu amesema hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani ya nafsi.

“Siwezi kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani…. 

#ThereIsNoPlaceLikeHome… Feels good to be Back…”ameandika Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mapema mwezi Februari mwaka huu mrembo huyo alitangaza kuihama CCM na kujiunga Chadema akisema “Nimeamua kufanya uamuzi wa kuhama chama cha Mapinduzi na hivi sasa nataka kuhamia Chadema. Sitaki ionekane kwamba labda nimepata hasira kulingana na hizi tuhuma za hapa katikati ambazo zimenikabili. Lakini nataka nionekane nimefanya maamuzi kama binadamu yeyote ambaye angeweza kufanya. 

Nadhani wote mnajua kuwa nilishawahi kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi, nilikuwa nalisema kwa kujiproud nikiwa nina uaminifu mkubwa kwamba mimi nitasimama kama kweli kada wa Chama cha Mapinduzi”

Comments