Mathayo 24:1-14
1) Yesu Akaenda zake, akatoka hekaluni; Wanafunzi Wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya Hekalu.
2) Naye akajibu akamwambia hamyaoni haya yote amini nawaambieni halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa ishara za mwisho wa nyakati
3) Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha wakisema tuambie mambo hayo yatakuwa lini ? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ?
4) Yesu akajibu akamwambia angalieni mtu asiwadanganye.
5) Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni kristo nao watadanganya wengi.
6) Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita angalieni msitishwe maana hayo hayana budi kutukia lakini ule mwisho bado.
7) Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa na ufalme kupigana na ufalme kutakuwa na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali
8) Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu mateso yatabiriwa
9) Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki nao wataua nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
10) Ndipo wengi watakapojikwaa nao watasalitiana na kuchukiana.
11) Na manabii wengi wa uongo watatokea na kudanganya wengi.
12) Na kwa sababu ya kuongezeka maasi upendo wa wengi utapoa.
13) Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka
14) Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo ule mwisho utakapokuja chukizo la uharibifu
************************
LUKA 21:1-19
1) Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina
2) Akamuona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili
3) Akasema hakika nawaambia huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;
4) Maana hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo kuangamizwa kwa hekalu Kwatabiriwa
5) Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu alisema
6) Haya mnayoyatazama siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa ishara na mateso
7) Wakamwuliza wakisema mwalimu mambo hayo yatakuwa lini ? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia ?
8) Akasema angalieni msije mkadanganyika kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ndiye tena majira yamekaribia basi msiwafuate hao.
9) Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina msitishwe maana hayo hayana budi kutukia kwanza lakini ule mwisho hauji upesi.
10) Kisha aliwaambia taifa litaondoka kupigana na taifa na ufalme kupigana na ufalme
11) Kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi na njaa na tauni mahali mahali na mambo ya kutisha na Ishara Kuu kutoka mbinguni.
12) Lakini kabla ya hayo yote hayajatokea watawakamata na kuwaudhi watapelekwa mbele ya masanagogi na kuwaua magerezani mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.
13) Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu.
14) Basi kusudieni mioyoni mwenu Kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;
15) Kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawatoweza kushindana nayo wala kupinga.
16) Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu na ndugu zenu na jamaa zenu na rafiki zenu nao watawafisha baadhi yenu.
17) Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu
18) Walakini Hautopotea hata unywele mmoja wa vichwa Vyenu.
19) Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu Unabii Wa Kuangamizwa YERUSALEMU.
*****************************
TIMOTHEO 3:1-9
1) Lakini ufahamu neno hili ya kuwa siku za mwisho kutakuwako na nyakati za HATARI.
2) Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe wenye kupenda fedha wenye kujisifu wenye kiburi wenye kutukana wasiotii wazazi wao wasio na shukrani wasaio safi,
3) Wasiopenda wa kwao wasiotaka kufanya suluhu wasingiziaji wasiojizuia wakali wasiopenda mema,
4) Wasaliti wakaidi wenye kujivuna wapendao anasa kuliko kumpenda mungu;
5) Wenye Mfano wa Utauwa lakini wakikana nguvu zake hao nao ujiepushe nao.
6) Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba watu na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mzigo ya dhambi waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
7) Wakijifunza siku zote ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
8) Na kama vile yane na Yambre Walivyopingana na musa vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli ni watu walioharibika akili zao wamekataliwa kwa mambo ya IMANI.
9) Lakini Hawataendelea sana maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote kama vile na mpumbavu wa hao walivyokuwa dhahiri Mausia Ya Paulo Na Timotheo.
**************
Hizo Ndizo Dalili Kuu Za Mwisho Wa Dunia Sio Kwamba Itakwisha Kwa Siku Moja Umeshuhudia Mwenyewe Matendo Yanayotokea Kwa Sasa.
Inadhihilisha kuwa tupo mwisho wa dunia Tuache Dhambi Ndugu Zangu Tumkumbuke Mungu Wetu Maana Yeye Ndio Kila Kitu Katika Maisha Yetu.
Josephat Charles Mtengwa
Imezaminiwa Na Roho Mtakatifu
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA