1st: Andika list ya viushindi vyako vidogo vidogo vya nyuma, note down your previous small victories. Hakika ukivikumbuka vitakutia nguvu ya kuendelea. Wewe Andika mfano umelipata division one form six huu ni ushindi, umewahi kuwa mfanyakazi Bora kazini kwako, wewe ni time manager mzuri, una marafiki wazuri na nk hivi viushindi vidogo ukiwa unavisoma baada ya muda vinakurudishia spirit ya kusonga mbele Tena.
2nd: Chukua kioo na jiangalie na sema maneno kama haya, am blessed, am talented, am favored, am chosen, am genius, am capable, am beautiful/handsome na mengine mengi inawezekana umekuwa ukiyasubiri kutoka kwa rafiki yako @nafanikiwa_inspiration aseme au @mwl_angelo aseme naomba leo hii ujiambie mwenyewe yanarudisha self image vizuri Sana. The Power of self affirmation and self talk.
3rd: Ongea na rafiki yako na mshauri wako, vizuri si lazima mzungumze kile kinachokufanya ukate tamaa bali mfanye mazungumzo tu mengine baada ya hapo utakuwa unajisikia tofauti.
4th:Jiulize kwa nini ulianza hicho unachotaka kukikatia tamaa, ukikumbuka tu kwa nini ulianza hakika utaendelea, pia angalia mangapi umevuka mpaka hapo kumbe hata hili linapita. Vimbunga vingine vinakuja kwenye maisha yetu si kuharibu bali ni kutusafishia njia zetu.
5th: Kwa imani yako pata muda mzuri wa peke yako sali, baada ya dua ama sala yako utarudi ukiwa ni mpya na Mwenye matumaini mapya kabsa. Cha kwanza ni kuamini kuwa hiki kitafanikiwa na cha pili ni tumaini kuwa kesho yetu ni kubwa hata kama Leo yetu ni nyembamba.
#MrBrandGroup #MrBrand
Imeandikwa Na Charles Nduku
Comments
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA