VITU VITAKAVYO KUSAIDIA KATIKA MAISHA YAKO

Mwisho wa siku ni mwanzo wa siku ya kesho, moja kati ya sehemu muhimu katika maisha yetu ni pamoja na kuwa mipango na ratiba zetu ambazo tunaziishi kwenye level ya siku, week, mwezi, miezi, mwaka na miaka. Hii inaweza kukusaidia hata wewe ndg yangu unaesoma hii meseji kwa namna gani unaipanga siku yako ya kesho, hizi ni baadhi ya hatua zinaweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine ili kesho yako iwe yenye mpangilio na yenye kuleta TIJA. 1st: Kabla hujaenda kulala hakikisha unajua kesho uanzia wapi kwa maana ya kujua majukumu yako ya kesho ni yapi, hii itakusaidia hata kukupa muda wa kuamka uamke saa ngapi ili ufanye nini na wapi. 

 2nd: Kuwa na ramani yako nzima ya siku, kuanzia asubuhi mpaka jioni wakati wa kurudi nyumbani, ukiwa na muda wa free usiutumie vibaya fanya kitu chenye kukujenga kuelekea malengo yako. Hii itakusadia kuwa na FOCUS na kile unachotaka kukipata maana unakuwa na plan nzima mkononi mwako. 3rd: Anza asubuhi na agenda ngumu ukiwa na nguvu na akili ikiwa haijachoka halafu baada ya agenda ngumu au agenda mama sasa zingine malizia ambazo hazikupi presha sana kuzikamilisha (Eat that Frog First Principle) 

 4th: Baada ya kuwa Routine yako mkononi sasa hapa zingatia muda moja ya changamoto kubwa hapa ni kuweza kupanga ila kushindwa kwenda na muda ili kuyafikia malengo yako ya siku. Time Management is the key to your personal schedule. 

 5th: Unaweza ukawa na notebook yako au diary ukimaliza ratiba moja kwenda nyingine unaweka tick......hii inakujenga sana psychologically kwani you feel succeeding and achieving so kufikia lengo la pili inakua rahisi/Self Motivation through Self Appreciation.

 6th: Ni asubuhi tu na jioni ndizo nyakati ambazo ziko nje ya uwezo wetu hatujui tutaamkaje kesho pia hatujui baada ya asubuhi jioni tutafika tukiwa na hali gani. #ThePowerofBranding #MrBrand #Read2Lead Imeandikwa Na Charles Nduku

Comments