Hongera Mbwana Samatta

- Klabu ya Aston Villa ya England, imekubaliana kila kitu na mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta. Samatta ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na leo asubuhi anatarajia kusafiri kutoka Dussedorf nchini Ujerumani kwenda Birmingham, England kwa ajili ya vipimo. Baada ya vipimo kukamilika, litafuatia suala la usajili wake na huenda kila kitu kikakamilika leo. - - Dau limeelezwa kuwa ni pauni milioni 10. Awali, ilielezwa Samatta angetua Norwich City au Newcastle, hata hivyo Aston Villa wameibuka na kumchangamkia. Kama atamalizana na Aston Villa, Samatta atakuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza soka katika Ligi Kuu England. - - Alianza kucheza nje ya Tanzania alipojiunga na TP Mazembe akitokea Simba na kuichezea kwa mafanikio hadi alipoamua kutoka nje ya bara la Afrika akijiunga na KRC Genk ambayo ameiwezesha kucheza Europa League, Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Comments